Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mchungaji Dkt. Msafiri Joseph Mbilu ameisihi Halmashauri ya Mipango na fedha  kuketi na kupitia mpango mkakakati wa Dayosisi  kwa umakini mkubwa kuchambua na kutoa maoni yenye tija  ili utekelezaji wake uweze  kuja kuwa  na tija.

Askofu Dkt Mbilu ametoa rai hiyo leo tarehe: 22/03/2022 wakati akifungua kikao cha Halmashauri hiyo ya Mipango na fedha ya Dayosisi kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano Utondolo Wilayani  Lushoto.

Halmashauri hiyo inajadili na kupitisha mpango mkakati wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, ili upelekwe kwenye Halmashauri Kuu ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki ili kuujadili na kuupitisha rasmi mpango mkakati  wa Dayosisi na baaadae uweze kutumika katika Dayosisi nzima. Mpango Mkakati huo ni wa kipindi cha miaka 5 kuanzia 2022 hadi 2026.

Katika ufunguzi Askofu Dkt Mbilu alihubiri neno la Mungu kutoka kitabu cha Injili ya Luka 14:28, na kuongeza kuwa ni imani yake utendaji kazi wao utampa  Mungu Utukufu kwani mpango huo utakuwa ni Dira ya Dayosisi.