Leo tarehe 13/02/2020 kumekuwa na mwendelezo wa semina ya uanzishwaji wa Kampuni ya uwekezaji ya Dayosisi ya Kaskazini Mashariki KKKT (NEDICO- North Eastern Diocese Investment Company) ambayo inatolewa katika awamu nyingine kwa mfululizo wa siku mbili 13-14/2020 na kuhusisha Wakuu wa Vituo, Waratibu wa Idara, Wachungaji kadhaa wa Sharika, Wakurugenzi, Wakuu wa Dinari na Uongozi wa Dayosisi.

 

Semina hiyo inaratibiwa na Ofisi Kuu ya DKMs KKKT na wawezeshaji  wa mafunzo toka  KKKT (LUICO- Lutheran Investment Company) inafanyika katika hostel ya Mbuyu Kenda , iliyopo Mkoani Tanga. Awali semina kama hii  ilifanyika Januari 17, 2020.