Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amewataka Wakristo kumpokea Yesu na kumkaribisha mioyoni mwao ili afanyike Nuru katika maisha yao na kuondoa giza na matendo yasiyofaa ambayo ni chukizo mbele za Mungu yaliyo tanda  katika ulimwengu na kuwasihi kumpokea  Yesu Kristo ambaye  ni  nuru ya ulimwengu.

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, amewataka wananchi wa Lushoto mjini kuchangamkia fursa za kibiashara katika maeneo yao ili kujikwamua kimaisha,kukuza uchumi wao na uchumi wa Wilaya ya Lushoto.

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch, Dkt Msafiri Joseph Mbilu amewataka wachungaji na watumishi  kutambua kua wanapoitwa kumtumikia Mungu katika huduma yao wanaitwa wao pamoja na wenzi wao ili kuibeba huduma hiyo ambayo Mungu amewaitia.

Ufunuo 14:13 “Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao”

Katibu Mkuu wa KKKT- Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mwl. Julius Madiga kwa niaba ya Uongozi wa KKKT- Dayosisi ya Kaskazini Mashariki anasikitika kutangaza kifo cha Mwj. Ridas Edward Jani kilichotokea usiku wa kuamkia  tarehe 17/12/2023 nyumbani kwa marehemu Majengo Juu Hale.