Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch. Dkt. Msafiri Joseph Mbilu leo tarehe 30/08/2021 amefanya ziara ya kikazi katika Shule ya Sekondari  Lwandai. Katika ziara hiyo Baba Askofu Mbilu alitembelea mazingira ya Shule na kupokea taarifa  iliyowasilishwa na Mkuu wa Shule hiyo, Mch. Daniel Mwarabu na waandamizi wa idara mbalimbali za shule hiyo.

Aidha Mhashamu Askofu alitembelea na kujionea miradi na kazi zinazoendelea katika Shule hiyo.
Katika ujumbe wake kwa jumuiya ya shule hii, Mhashamu Askofu Dkt. Mbilu aliwapongeza wafanyakazi kwa kazi kubwa wanazofanya katika Shule hii hasa utoaji wa taaluma unaodhihirishwa na ufaulu mzuri wa madarasa  yaliyofanya mitihani ya Taifa mwaka jana (kidato cha II & IV) ambapo hakukuwa na daraja sifuri na wengi wa wanafunzi kufaulu kwa kiwango cha daraja la  III hadi I. Aliwatakia baraka za Mungu na kuwapa wito wa kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuitangaza shule hiyo vema kwa wadau wa elimu katika jamii .