
Leo tarehe 17/07/2022 imekuwa siku ya baraka tele kwa washarika wa Jimbo la Kaskazini ,Usharika wa Mlalo kwani vijana wapatao 116 walipata kipaimara na wanne 4 kati yao walibatizwa.

Katika Ibada hiyo Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu ndiye aliye ongoza Ibada hiyo, huku Liturgia ikiongozwa na Msaidizi wa Askofu KKKT-DKMs Mch. Michael Mlondakweli Kanju.


Katika Risala ya vijana hao waliobarikiwa iliyosomwa mbele ya Baba Askofu Dkt. Msafiri Mbilu vijana hao wametambua jitihada za Baba Askofu pamoja na wasaidizi wake katika kusimamia mambo ya Elimu na Afya. Hata katika kipindi hiki ambacho Dayosisi inakabiliana na deni bado wameona na kushuhudia kazi za maendeleo zikiendelea kufanyika.

Wameeleza kujisikia fahari kuona shule za Dayosisi (Lwandai na Bangala) zikiboreshwa na kuvutia wanafunzi wengi zaidi. Huku wakitambua jitihada za kukifufua kilichokuwa Chuo cha SEKOMU,kwa hatua za awali za kuanzishwa kwa Chuo cha Kati cha Kolowa Technical Training Institute (KOTETI) kitakachotoa kozi ya famasia.








