Msaidizi wa Askofu Mteule wa KKKT- Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch.Michael Mlondakweli Kanju amewapongeza Wachungaji wanawake  wa Dayosisi ya Kaskazini Mashariki kwa umoja wao katika kusaidiana,Kuhamasishana, kutembeleana katika maeneo yao ya kazi pamoja na kuombeana, kwa kuwa ni wito  walioitiwa.


Mch Kanju ameyasema hayo katika ufunguzi wa mkutano mkuu wa tatu wa wanawake wachungaji WOPA ulio fanyika katika ukumbi wa mikutano Utondolo  Wilayani Lushoto Mkoani Tanga, wenye lengo la kupata taarifa ya mpango kazi wa kipindi cha miaka miwili iliyopita pamoja na kuchagua viongozi wapya wa umoja huo. Ambapo pia  aliwapongeza kwa namna wanavyo endesha shughuli zao na kuwataka kujiwekea malengo katika mambo wanayotaka kuyafikia.Huku akiwahakikishia kuwa uongozi upo tayari kushirikiana nao.


Pamoja na mambo mengine yaliyo jadiliwa mkutano huu umekuwa na ajenda  ya uchaguzi ambapo waliochaguliwa kuongoza umoja huo wa wachungaji wanawake ni Mch.Nuru Mwakapusia-Mwenyekiti, Mch.Lemmi Kakai Katibu na Mch.Vengeline Mnyalapi - mtunza hazina.


Uongozi uliomaliza muda wake ni Mch.Neema kamendu aliyekuwa mwenyekiti,Mch Happyness Diu Katibu na Mch Joyce Kibanga aliyekuwa mtunza hazina.
Umoja huu unashirikiana na wachungaji wanawake kutoka ndani ya KKKT, CCT na makanisa ya Kilutheri yaliyoko nje ya Nchi.