Mchungaji Issai Amasia Mweta ameingizwa kazini kuwa Mkuu wa Jimbo la Kusini KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki . Mch Issai Amasia Mweta alichaguliwa katika mkutano Mkuu uliofanyika Katika Kanisa Kuu Lushoto Novemba 25 hadi 27 mwaka jana na ameingizwa kazini na Baba Askofu Dkt Msafiri Joseph Mbilu leo tarehe 30/05/2021 katika Usharika wa Soni.