MATUKIO KATIKA PICHA:- Tarehe 22/10/2023 ilikuwa siku ya furaha na baraka tele kwa washarika wa Jimbo la Kusini Usharika wa Manka ambapo, Jumla ya Vijana wa Kipaimara 60 wamebarikiwa katika Jimbo la Kusini Usharika wa Manka huku Vijana hao wakitoa shukrani zao kwa Baba Askofu Dkt Msafiri Joseph Mbilu kwa kupata nafasi ya kufundishwa mafundisho ambayo yameimarisha Imani yao huku wakisema kupitia mafundisho hayo mazuri ya neno la Mungu wamepata msingi imara wa kiroho na kimwili.
 
Aidha Vijana hao wameahidi mbele ya Baba Askofu Dkt. Mbilu pamoja na wazazi na washarika walioshiriki katika Ibada hiyo kua watakuwa mstari wa mbele katika kuiimarisha Dayosisi kwa kufanya shughuli mbalimbali za Dayosisi ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanachangia deni linaloikabili Dayosisi
 
Katika Ibada hiyo Vijana hao walitoa kiasi cha Tsh 120,000 kwaajili ya kuchangia ulipaji wa deni la Dayosisi na Tsh 60,000 kwaajili ya maendeleo ya Jimbo la Kusini ambapo pia waliomba kuungwa mkono na wazazi,walezi pamoja na washarika walioshiriki katika Ibada hiyo na kufanikiwa kukusanya jumla ya Ths. 532,000/= ambapo fedha hizo zimeelekezwa katika kulipa deni la Dayosisi.
Awali Ibada hiyo ya Kipaimara ilitanguliwa na Ibada iliyokuwa na tendo la kuweka jiwe la Msingi la Kanisa la Mtaa wa Kwemaluli.