Uncategorised
- Details

Leo tarehe 04/06/2025 Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, ametembelea Kituo cha Irente Children’s Home kwa lengo la kukagua zoezi la ukaratabati wa Miundombinu ya bweni la wanafunzi wanaosoma kozi ya Elimu ya Awali na Malezi Bora katika kituo hicho kinacho milikiwa na KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki.
- Details

KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, inayomiliki Hospitali ya Kilutheri Bumbuli (Bumbuli Lutheran Hospital) imeendelea kufanya maboresho katika Hospitali hiyo baada ya hivi karibuni kutoa mashine ya usingizi (Anesthesia Machine) pamoja na vifaa tiba vingine vya kisasa ambavyo vitasaidia kuendelea kuboresha huduma ya Afya Hospitalini hapo.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Huduma za Jamii wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mwl. Afizai Elisa Vuliva, wakati akikabidhi mashine hiyo kwa uongozi wa Hospitali ya Bumbuli huku akiwataka kutunza mashine hiyo pamoja na vifaa vingine vilivyo pelekwa hospitalini hapo kutoka kwa Shirika la GIZ.
- Details

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Dkt. Msafiri Joseph Mbilu yupo katika ziara ya kikazi Nchini Ujerumani ambapo ameambatana na Dean Mteule Frank Mtangi pia wamepata wasaa wa kutembelea Jimbo la Staaken kwenye Jiji la Berlin.
Page 10 of 125


