

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, leo tarehe 30/11/2021 amehitimisha ziara yake ya siku mbili katika Usharika wa Pongwe, Jimbo la Pwani.

Baba Askofu Dkt. Mbilu amehitimisha ziara yake hiyo leo kwa kuongoza Ibada ya uwekwaji wa jiwe la msingi la Kanisa katika Usharika wa Pongwe, Mtaa wa Machemba pamoja na ufunguzi wa Kanisa katika Usharika wa Pongwe, Mtaa wa Kilapula.

Katika Usharika wa Pongwe, Mtaa wa Machemba, Baba Askofu ametoa kiasi cha Tsh 100,000 kuunga mkono kazi ya Bwana inayoendelea katika Mtaa huo,kwa upande mwingine Eng. Benedict Lema ametoa kiasi cha Tsh 2,000,000 milioni mbili kwaajili ya ujenzi wa Kanisa hilo unaoendelea.


MKUU WA JIMBO LA PWANI, MCH. THADEUS A. KETTO
Msafara wa Baba Askofu chini ya Mkuu wa Jimbo la Pwani Mch. Thadeus A. Ketto wameahidi kutoa kiasi cha Tsh. 1,150,000 zitakazo tumika katika ujenzi huo wa Kanisa unaoendelea.


Hata hivyo mara baada ya Ibada katika Usharika wa Pongwe, Mtaa wa Machemba, Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu alijumuika na washarika wa Usharika wa Pongwe, Mtaa wa Kilapula kwenye Ibada ya Shukrani ya ufunguzi wa Kanisa.Baba Askofu amewapongeza washarika wa mtaa huwa wa Kilapula kwa ujenzi mzuri wa nyumba hiyo ya Ibada kwani imejengwa katika kiwango kizuri na litadumu kwa kipindi kirefu.

Mtaa wa Kilapula ulianzishwa tarehe 20/08/2008 ukiwa chini ya Mtaa wa Kilole uliokua katika Usharika wa Kana chini ya Mch. Lewis Shemkala na Mitaa hii ilitunzwa na Mwj Hemba.

Washarika wa Mtaa wa Kilapula hawajkusita kutoa shurani zao za pekee kwa watumishi waliowatunza kiroho katika ujenzi huo wa Kanisa.
- Mch. Lewis Shemkala Mtaa huo ulipokuwa chini ya Usharika wa Kana na yeye aliwezesha upatikanaji wa eneo hilo.
- Mch Neema Kamendo
- Mch Dkt Msafiri Mbilu
- Mch.Thadeus A. Ketto.
Hadi leo hii Mtaa huo wa Kilapula una jumla ya Wakristo 201, watu wazima ME. 52, KE 75 JUMLA = 127, na Watoto ME 32 KE 42 JUMLA 74.Ikumbukwe hapo jana Baba Askofu Dkt. Mbilu aliongoza Ibada ya ufunguzi wa darasa la Watoto wa Shule ya Jumapili,katika Usharika wa Pongwe, Mtaa wa Saruji.na ujenzi wa Darasa hilo ulianza mwezi June,2021 chini ya Mch. Nkanileka Chedi.
Kwa upande mwingine Baba Askofu amepongeza vikundi vya kwaya vya Usharika wa Pongwe na Mitaa yake kwa ujumla kwa uimbaji mzuri upigwaji wa vyombo vya muziki (LIVE) kwani hiyo ndio maana ya kumwimbia Mungu wimbo mpya kila siku.

Hakusita kukemea uimbaji wa kutumia flash yaani matumizi ya nyimbo zilizo rekodiwa tayari kwani njia hiyo inadumaza uimbaji, walimu wa muziki wamekumbushwa kutunga nyimbo nzuri zenye maneno mazuri na zinazoendana na nyakati.




