Nyumba hubarikiwa ukaamo,Yesu,uliye mpenzi wa moyo,wakukaribishapo kwa furaha,uliye mgeni wa heshima kuu.mioyo yetu inapokupenda na macho Yote yakungojapo, midomo yote ikuulizapo, na watu wote wanapokutii.

Askofu Msaatafu Joseph Jali amewashukuru wana KKKT-Dayosisi ya Kaskazini kwa itikio lao kubwa katika utoaji wa michango itakayo wezesha kuweka alama ya maadhimisho hayo katika shule ya Bangala Lutheran Junior Seminary kwa kumalizia ujenzi wa bwalo katika shule hiyo uliosimama kwa muda mrefu.

Lengo la Baba Askofu Mstaafu JMzee Joseph Jali nikuona Bangala Lutheran Junior Seminary inasimama upya na kurudi katika hali yake ya kawaida hivyo ameendelea kuwaalika wana Dayosisi rafiki ndugu na jamaa katika kuwezesha lengo la maadhimisho hayo.

Shukrani hizo amezitoa leo tarehe 19/12/2021 kwenye Ibada ya maadhimisho ya Jubilee ya kumbukumbu ya miaka 60 ya ndoa yake na Bibi Sarah Jali.

Kwa upande mwingine Askofu Mstaafu Dkt. Paul Akyoo wa KKKT-Dayosisi ya meru ambaye ndiye aliye ongoza Ibada hiyo amesema kuwa siku hii ya leo tunaposherehekea kumbukumbu ya mika ya 60 ya wazee na wazazi wetu tunakila sababu ya kumshukuru Mungu, ndugu zangu ndoa si jambo rahisi kamaambavyo wengi wao wanaweza kufikiri,ndoa ni safari, ndoa ni kipawa, ndoa ni baraka lakini pia ndoa ni neema itokayo kwa Mungu.

Ameongeza kuwa ndoa sio chukua twende bali ndoa inahitaji hekima,busara,utulivu na usikivu ndio maana tunahitaji kumtukuza na kumhimidi Mungu.

Askofu Mstaafu Jali na Bibi Sarah Jali walifunga ndoa tarehe 08/05/1960 na aliye funga ndoa hiyo ni Hayati Mch. Michael Mhombo katika Usharika wa Bungu-Lutindi.