
Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu ameongoza Ibada ya mazishi ya marehemu Mzee Enock Nickodem Magombya Leo tarehe 22/12/2021 katika Usharika wa Hale Jimbo la Tambarare.


Marehemu Mzee Enock Magombya aliitwa mbinguni asubuhi ya tarehe 19/12/2021 akiwa kwenye viwanja vya Kanisa Kuu (Cathedral) Lushoto akijiandaa kushiriki Ibada ya maadhimisho ya Jubilee ya kumbukumbu ya miaka 60 ya ndoa ya Askofu Mstaafu Mzee Joseph jali.

wakati anasalimiana na watu mbalimbali alijisikia vibaya na wakati akipatiwa usaidizi aliitwa mbinguni.

Katika mahubiri ya Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amesema kuwa kila mtu anamahali pake pakufia na wengine wamefia katika maeneo magumu na yasiyo mpa Mungu utukufu ila Mzee Magombya yeye amechagua kufia katika viwanja vya Kanisa Kuu (Cathedral) Lushoto sehemu inayo unganisha Sharika zote za KKKT-DKMs.

Kwa upande mwingine Askofu Mstaafu Mzee Joseph Jali amesema kuwa Marehemu Mzee Enock Magombya alikuwa rafiki yake wa kweli na alipata nafasi ya kufanya nae kazi akiwa kiongozi katika ngazi ya Dayosisi ikiwemo ujenzi wa Kanisa la Usharika wa Hale.

Alizaliwa mwaka 1936 katika Kijiji cha Ikuna Wilayani Njombe mkoani Njombe,katika uhaiwaki aliwahi kuwa mwalimu wa kwaya, Mwinjilisti wa kujitolea kisha alienda masomo katika chuo cha mwika na hivyo kuwa mwinjilisti kamili,mnamo mwaka 1999 alistaafu huduma hiyo ya uinjilisti.



Maisha yake ya ndoa alifunga ndoa mwaka 1962 kijijini kwao Ikuna na mkewe Alatukolela Petro Ngimbuchi walijaliwa Watoto 8 na jumla ya wajukuu 18.


