
Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mchungaji Dkt. Msafiri Joseph Mbilu ameisihi Halmashauri ya Mipango na fedha kuketi na kupitia mpango mkakakati wa Dayosisi kwa umakini mkubwa kuchambua na kutoa maoni yenye tija ili utekelezaji wake uweze kuja kuwa na tija.

Askofu Dkt Mbilu ametoa rai hiyo leo tarehe: 22/03/2022 wakati akifungua kikao cha Halmashauri hiyo ya Mipango na fedha ya Dayosisi kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano Utondolo Wilayani Lushoto.

Halmashauri hiyo inajadili na kupitisha mpango mkakati wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, ili upelekwe kwenye Halmashauri Kuu ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki ili kuujadili na kuupitisha rasmi mpango mkakati wa Dayosisi na baaadae uweze kutumika katika Dayosisi nzima. Mpango Mkakati huo ni wa kipindi cha miaka 5 kuanzia 2022 hadi 2026.

Katika ufunguzi Askofu Dkt Mbilu alihubiri neno la Mungu kutoka kitabu cha Injili ya Luka 14:28, na kuongeza kuwa ni imani yake utendaji kazi wao utampa Mungu Utukufu kwani mpango huo utakuwa ni Dira ya Dayosisi.


