
Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Fungamano la Makanisa ya Kilutheri Duniani (LWF) Mch. Anne Burghardt katika Ofisi za Makao Makuu ya KKKT (Arusha) ambapo Katibu Mkuu huyo yupo Nchini Tanzania kwa ziara ya Kikazi katika Kanisa la KKKT.
Aidha, Askofu Dkt. Mbilu ni mmoja kati ya wanakamati ya Ibada na Muziki ya Fungamano la Makanisa ya Kilutheri Duniani (LWF) inayoandaa Mkutano Mkuu utakaofanyika Nchini Poland mwakani
Kamati hii iliundwa mwaka 2021 na ofisi ya Katibu Mkuu wa Fungamano la Makanisa ya Kilutheri Duniani ambayo makao Makuu yake yapo Geneva Uswis. Kamati hii ina wajumbe kumi kutoka Ujerumani,Canada,Norway,Hungary,Poland,Hong Kong,USA,Brazil,Switzeland na Africa ambapo mjumbe muwakilishi ni Askofu Dkt. Msafiri Mbilu.


