
Katika jitihada za kuhakikisha kiwanda cha uchapishaji cha Vuga Press Publishing House kinacho milikiwa na KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki kinaingia katika soko la ushindani Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu leo tarehe 15/06/2022 amekutana na kufanya mazunguzo na mtaalamu wa maswala ya uchapishaji,Masoko,Ujasiriamali na utawala katika biashara na viwanda kutoka Nchini Holland,

bwana Hans Baljet ambapo wamezungumza juu ya upatikanaji wa mitambo ya kisasa itakayo saidia ufanyaji wa kazi nyingi kwa kutumia muda mfupi na upatikanaji wa mitambo inayotumia teknolojia ya kisasa ili kurudisha sifa na heshima ya kiwanda hicho kikongwe kilicho anzishwa mwaka 1912.




