MATUKIO KATIKA PICHA: Harambee ya kuchangia kazi za maendeleo na vituo vinavyotoa huduma kwa watu wenye mahitaji maalum (Diakonia) kwa Dini zote vinavyomilikiwa na KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, iliyofanyika tahere 15/10/2023, katika ukumbi wa Regal Naivera Tanga.

Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mjini Mhe. James Wilbert Kaji

Mgeni Rasmi alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Waziri Waziri Kindamba ambaye aliwakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mjini Mhe. James Wilbert Kaji. Harambee hii imefanikiwa kwa kupata ahadi ya shilingi Milioni themanini na moja laki tano na kumi na tano elfu na mia nane (Tsh, 81,515,800) na Fedha Taslimu ilipatikana shilingi Milioni sabini na sita laki tatu na hamsini na tatu (Tsh.76,353,000) na kufanya jumla kuu kuwa shilingi Milioni mia moja na hamsini na saba, laki nane na sitini na nane elfu na mia nane (Tsh.157,868,800).