
Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch, Dkt Msafiri Joseph Mbilu amewataka wachungaji na watumishi kutambua kua wanapoitwa kumtumikia Mungu katika huduma yao wanaitwa wao pamoja na wenzi wao ili kuibeba huduma hiyo ambayo Mungu amewaitia.

Askofu Dkt. Mbilu ameyasema hayo kwenye Mkutano uliyowakutanisha Wachungaji, Mashemasi na wenzi wao uliofanyika katika Jimbo la Tambarare Usharika wa Korogwe na kuongeza kua maisha ya watumishi ni lazima yawe mazuri naya mfano mzuri kwa watu wanaowaongoza .

MCH. LEWIS SHEMKALA PAMOJA NA MWENZI WAKE.
Kwa upande wake Mch Gibson Aggrey amesema kuwa amefurahishwa na mkutano huo wa Wachungaji na wenzi wao huku akisema kua kazi ya wito sio kazi ndogo bali ni kazi kubwa inayo hitaji kutiwa moyo na ameahadi baada ya mkutano huo kumtumikia Mungu kwa upya kutokana na mengi aliyojifunza kupitia mada mbailimbali zilizo wasilishwa katika mkutano huo.

Naye Shemasi Rehema Mbura, amesema kua kwa mafundisho waliyoyapata katika mkutano huo wameweza kujengwa na kuimarishwa kwa upya hivyo ana imani kwamba watumishi hao watakapo rudi katika vituo vyao vya kazi wataendelea kusimama imara katika utumishi wao na ndoa nyingi zitakua zimepona na kuimarika.

MCH. JEREMIAH MBOKO PAMOJA NA MWEZI WAKE.
Kwa upande wake Mchungaji John Ndimbo akizungumzia juu ya mada iliyowasilishwa na Baba Askofu Dkt Msafiri Joseph Mbilu isemayo NYUMBA YA MCHUNGAJI NAFASI YA MWENZI NA MTOTO, Mch. ndimbo amesema kuwa nyumba ya mtumishi ni kimbilio la waumini huku akikiri kujifunza vema juu ya ulimwengu unaobadilika na namna ya kuishi na waumini ambao hubadilika.

MKUU WA JIMBO JIPYA LA MAGHARIBI MCH. ISHMAEL REUBEN NGODA NA MWENZI WAKE.

