Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, amewataka wananchi wa Lushoto mjini kuchangamkia fursa za kibiashara katika maeneo yao ili kujikwamua kimaisha,kukuza uchumi wao na uchumi wa Wilaya ya Lushoto.
Hayo ameyasema wakati akifungua vibanda 17 vya biashara,vinavyo milikiwa na KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki,,vilivyopo nje ya Ofisi Kuu ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki leo Tarehe 20/12/2023, huku akiahidi pamoja na changamoto ya madeni yanayoikabili Dayosisi bado kazi za maendeleo zitaendelea kufanyika.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Mhe. Kalist Lazaro, amempongeza Askofu Dkt. Mbilu pamoja na Wanadayosisi kwa kazi kubwa ya ujenzi wa vibanda hivyo vya biashara.
Aidha Mhe. Kalist ametoa ahadi ya kufunga taa za barabarani na kuunganisha Barabara ya kutoka katika vibanda hivyo hadi stendi ya mabasi ya Wilaya ya Lushoto kwa kiwango cha lami ifikapo 2024.