Leo tarehe 10/01/2021 Askofu Mteule Mch Dkt Msafiri Joseph Mbilu mara baada ya Ibada katika Usharika wa Kana Jimbo la Pwani,amepata nafasi ya kufanya kikao na baadhi ya wazee wa Kanisa na Wazee maarufu wa Jimbo la Pwani. Kikao kilifanyika katika hostel ya Mbuyu Kenda Tanga lengo likiwa ni kupata maoni ya wazee hao juu ya namna bora ya kuiendeleza na kuiimarisha hostel ya Mbuyukenda.

Pia ilitolewa sadaka maalumu kama alama ya kuimarisha hostel ya Mbuyu Kenda inayo milikiwa na Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMS).

Wazee hawa walipata nafasi ya kulizunguka eneo la Mbuyu Kenda, kuzuru hostel na eneo lililokuwa na Kanisa. Baada ya kuona hali halisi walitamani maeneo baadhi yafanyiwe ukarabati wa dharura na kwa kuunga mkono walichangia taslimu fedha za Kitanzania Tsh. 1,060,000/= na kama haikutosha walimshukuru Mungu kwa kuwakutanisha Mbuyu Kenda kwa kutoa sadaka Tsh. 159,700/=