Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, (KKKT-DKMs) Mch Dkt. Msafiri Josephu Mbilu, amewataka Wanaume wa KKKT- Dayosisi ya Kasikazini Mashariki kujitoa katika kukamilisha mipango na malengo waliyojiwekea katika mwaka wao huku akiwataka kuwa mstari wa mbele katika kusimamia maadili mema  ikiwa ni pamoja na kukemea ndoa za jinsia moja,  huku akiwataka wanaume wa Dayosisi hiyo kijitoa na  kuhudhuria katika Ibada na kushiriki katika maswala mazima ya uimbaji wa kwaya.

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt Msafiri Joseph Mbilu, leo tarehe 16/03/2024, ameongoza Ibada ya ufunguzi wa  Usharika  mpya Mteule wa Saunyi uliopo katika Jimbo la Magharibi, Ibada iliyoambatana na tendo la kuwabariki vijana wa Kipaimara 201 pamoja na kufungua  nyumba ya Mtumishi.

KATIKA PICHA: Ibada ya Jumapili ya tarehe 10/03/2024 kutoka Usharika wa St. Marien Minden nchini Ujerumani, ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu nchini humo.
Pamoja na mambo mengine yaliyojadiliwa katika Usharika huo Baba Askofu pamoja na mwenyeji wake wamekamilisha maandalizi ya ziara ya Vijana 11 kutoka katika Dayosisi yetu watakaotembelea nchi ya Ujerumani kuanzia tarehe 14. Aprili hadi tarehe 6. Mei 2024.
Vijana hao11 kutoka KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Usharika wa Mtae watakuwa na Kongamano la maswala ya Maji nchini Ujerumani. Kongamano hili litasimamiwa na Usharika wa St. Marien Minden.

Mwendelezo wa Ziara ya Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, tarehe 08/03/2024 amefanya ziara katika Jimbo la Vlotho nchini Ujerumani lenye urafiki na Jimbo la Tambarare la KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki. KATIKA PICHA, ni miongoni mwa Wajumbe wa Kamati ya Uhusiano chini ya Mwenyekiti wao Mch. Markus Freitag.(wa kwanza kutoka kulia).

Mwenyekiti wa Undugu kati ya Jimbo Vlotho nchini Ujerumani na  KKKT-DKMs Jimbo la Tambarare ,Mch. Markus Freitag (wa kwanza kutoka kushoto), mwenzi wa Askofu Dkt. Mbilu Mwl. Marry Jally (wa pili kutoka Kushoto), Askofu Dkt. Msafiri Mbilu (wa tatu kutoka Kushoto) pamoja na mwezi Mwenyekiti wa Undugu Mch. Markus Freitag, (wa nne kutoka Kushoto).