Tarehe 19 Juni 1963, Kanisa la Usambara - Digo na makanisa mengine sita ya Kilutheri yaliungana na kuunda Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania . Leo hii KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMs) yenye Makao Makuu Wilayani Lushoto Mkoani Tanga ni miongoni mwa Dayosisi 28 za KKKT. Dayosisi inaitwa hivyo kwakuwa inapatikana Kaskazini Mashariki mwa Tanzania katika Mkoa wa Tanga. Kwahiyo KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMs) ni taasisi ya kidini iliyosajiliwa tarehe 19 Juni 1963 na Makao yake Makuu yapo Wilaya ya Lushoto Mkoa wa Tanga. Dhamira ya KKKT-DKMs ni kufundisha na kuhubiri neno la Mungu na kutoa huduma nzuri za kiroho, kimwili, kiakili, kiuchumi na kijamii kwa watu wote. Taasisi hii inatoa tangazo la kazi kwa nafasi moja ya MRATIBU WA HUDUMA YA MTOTO NA KIJANA (PROJECT COORDINATOR) kwa vijana wote (Wakristo)
NAFASI NA WAJIBU WA MRATIBU WA HUDUMA YA MTOTO NA KIJANA (PROJECT COORDINATOR).
1.1 CHILD AND YOUTH DEVELOPMENT CENTER COORDINATOR (CYDC)- MRATIBU WA KITUO CHA MAENDELEO YA MTOTO NA KIJANA.
Mratibu wa Kituo cha Maendeleo ya Mtoto na Kijana ni mwajiriwa wa Kanisa na atatumika katika kituo cha maendeleo ya Mtoto na kijana (KKKT – SINDENI BWAWANI – TZ1212) kilichopo Sindeni – Wilaya ya Handeni. Katika utendaji wake wote wa majukumu /wajibu atawajibika kwa Mchungaji kiongozi na kusimamiwa na Kamati ya huduma ya Mtoto. Atasimamia utendaji wa watendakazi wengine katika kufanikisha shughuli za maendeleo ya ujumla ya Mtoto na kijana. Atasimamia maono ya maendeleo ya ujumla ya Mtoto na kijana na amali za huduma wakati wote wa Uhai wa kituo cha Huduma ya Mtoto.
Kazi muhimu na wajibu wa Mratibu wa Kituo Cha Maendeleo Ya Mtoto Na Kijana ni kama ifuatavyo:
- Atamshuhudia Yesu Kristo kwa uaminifu na kuwa mtetezi wa watoto na vijana.
- Kuandaa mpango wa mwaka wa mshirika-mwenza wa kituo cha maendeleo ya Mtoto na kijana kwa kushirikiana na wadau wote na kuwasilisha kwa Kamati ya Huduma ya Mtoto kwa uthibitisho na kuidhinishwa na uongozi wa Kanisa.
- Kuingiza na kusimamia utekelezaji wa mpango wa mshirika-mwenza kama ilvyoidhinishwa Kwenye mfumo wa Compassion Connect.
- Kujaza taarifa za mahudhurio za mlengwa mmoja mmoja katika mfumo wa taarifa wa Compassion (Compassion Connect)
- Kusimamia na kuratibu shughuli zote za watendakazi wengine na watu wanaojitolea katika kituo cha maendeleo ya Mtoto na kijana.
- Kuwasilisha taarifa ya kimaandishi ya utendaji na maendeleo ya kituo kwa kamati, uongozi wa Kanisa na huduma ya Compassion International Tanzania kama itakavyo takiwa kwa pande zote husika.
- Kuhakikisha ripoti zote za watendakazi wengine zinaandaliwa na kuwasilishwa kwa wakati na ubora unaotakiwa.
- Kuhakikisha kuwa taarifa zote za fedha na Watoto zinatunzwa vizuri na kuhuishwa kila mara zinapohitajika.
- Kutunza kitabu cha hundi cha kituo cha Maendeleo ya Mtoto na kijana na kupitisha malipo yote sambamba na maelekezo yaliyotolewa na kamati ya kituo na kulingana na miongozo ya kifedha ya Ushirikawenza.
- Kushiriki katika zoezi la usaili wa kuwapata watendakazi wengine wote wa kituo kwa kutoa maoni ya kitaalamu kuhusu nafasi hizo.
- Kuhakikisha mazingira ya walengwa kituoni ni salama kwao kujifunza na kushiriki katika programu zote za kituo.
- Kusimamia na kuwa mwangalizi mkuu wa utekelezaji wa mitaala yote inayotumika kituoni.
- Kusimamia shughuli zote za ufundishaji na waalimu wa walengwa.
- Atakuwa miongoni mwa walimu wa walengwa
- Kuandika Maandiko mbalimbali na kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo katika jamii kwa ajili ya mahitaji mbalimbali ya watoto, wazazi na kituo kwa ujumla.
- Kuhamasisha upatikanaji wa raslimali za ndani kwa ajili ya miundombinu inayohitajika kwa walengwa kujifunza.
- Kutathmini maendeleo ya watendakazi wengine wa kituo cha Huduma ya Mtoto na kuwasilisha maoni yake kwa kamati ya kituo.
- Kufuatilia kwa karibu maendeleo ya kiroho, kiafya, kielimu na kijamii ya mlengwa mmoja mmoja aliye katika programu.
- Kutembelea walengwa mashuleni na nyumbani na kuchukua hatua stahiki pale inapobidi.
- Atawajibika kwa matokeo tarajiwa ya walengwa, viashiria vya utendaji na matokeo ya ukaguzi, kwa mujibu wa mwongozo.
- Kuhakikisha walengwa wote wanaaandika barua kwa wafadhili wao kwa wakati na viwango vinavyotakiwa.
- Kuhakikisha kuwa taarifa zote za watoto na Kanisa zilizoko katika mfumo wa taarifa wa Compassion connect ni sahihi na zimehuishwa.
- Kuhakikisha zawadi zilizotumwa na wafadhili zinawafikia walengwa kwa wakati na kwa asilimia mia moja.
- Kushiriki katika mafunzo yanayoandaliwa kwa ajili ya huduma ya mtoto na vijana.
- Kuwasaidia watendakazi wengine wa Kituo na kushirikishana wajibu wao pale inapohitajika. Hii ni pamoja na kuhakikisha watendakazi wapya wanajua majukumu yao Kituo cha huduma ya Mtoto.
- Kutoa taarifa kwa kamati ya Huduma ya Mtoto, juu ya ubadhilifu wa fedha au tabia isiyoridhisha kwa mmojawapo wa Watendakazi wengine wa Kituo.
- Kuhakikisha watoto walioandikishwa katika Kituo kwa ajili ya ufadhili ni wale tu wanaokidhi vigezo vilivyowekwa katika Ushirika-wenza.
- Kuendesha vikao vya watendakazi mara moja kwa mwezi au zaidi pale inapobidi.
- Kushiriki kikamilifu Ibada za kila siku asubuhi pamoja na watendakazi wote kabla ya kuanza kazi.
- Kuratibu vikao na mafunzo kwa wazazi kwa kushirikiana na uongozi wa Kanisa pamoja na kamati ya wazazi kwa lengo la kuhamasisha watu hao kuhusika na maendeleo ya watoto.
- Kuandaa mpango na kuratibu uchunguzi wa Afya kwa ajili ya watoto/vijana katika Kituo
- Kuwafahamu watoto na walezi wenye mahitaji maalumu ya kiafya na kuandaa mpango wa utendaji kazi kwa kushirikiana na wadau wengine.
- Kuratibu ugawaji wa misaada na matunzo ya tiba wanayopatiwa walengwa waliotambuliwa.
- Kutembelea watoto/vijana majumbani na kutoa ushauri nasaha kwa watoto na walezi wenye mahitaji ya kuhudumiwa kwa tiba.
- Kufuatilia mwelekeo wa maswala yahusuyo Afya na kutoa taarifa kila mwezi kwenye uongozi wa huduma ya Mtoto na Ofisi ya nchi ya Compassion.
- Kuandaa mpango na kuratibu mafunzo, maelezo, elimu na mawasiliano yahusuyo afya pamoja na lishe.
- Kutambua na kushirikiana na asasi mbalimbali za Afya kwa lengo la kupata ushauri wa kitaalamu na uboreshaji wa shughuli za Afya chini ya ushauri wa uongozi wa huduma ya Mtoto.
- Atafanya kazi nyingine za kiofisi kama atakavyopangiwa na uongozi wa Kanisa.
1.2 SIFA ZA MRATIBU WA KITUO CHA MAENDELEO YA MTOTO NA KIJANAELIMU:
- Shahada ya Kwanza (kutoka kwenye chuo kinachotambulika/kukubalika na Serikali).
- Elimu katika maeneo ya Uongozi/utawala, Usimamizi wa biashara, maendeleo ya jamii, Maendeleo ya watoto, Theolojia, Ualimu na Sosholojia.
1.3 UJUZI/UFAHAMU/SIFA NYINGINE:
- Usimamizi wa Miradi, Uhamasishaji wa rasilimali na Uongozi.
- Mkristo aliyeokoka na kujitoa kwa Bwana Yesu; mwenye maisha ya Ushuhuda ya kila siku. Mwenye moyo wa kujitoa, kutumika kanisani na mpenda maendeleo, anayependa kufanya kazi na watoto na vijana kutoka katika mazingira magumu.
- Umri kuanzia miaka 25 na si zaidi ya miaka 40.
NAMNA YA KUTUMA MAOMBI.
Maombi yote yatumwe kwa
Katibu Mkuu KKKT-DKMs
S.L.P 10,
LUSHOTO TANGA
Kupitia email ya : This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
1.Barua ya maombi iambatanishwe na nakala za vyeti vya Elimu, wasifu wa mwombaji (Cv), cheti cha kuzaliwa, na nakala za vyeti vyote vya ujuzi mbalimbali (kama unavyo).
2.Barua ya utambulisho kutoka kwa Mchungaji wa Kanisa unaloabudia kwa sasa (Lazima)
3.Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 31/03/2025
4.Waombaji watakaokidhi vigezo ndio watakaoitwa kwenye usaili (Interview)
5.Tarehe ya usaili watajulishwa kwa njia ya simu