Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheru Tanzania , Askofu Dkt.Fredrick Shoo. amewasili Wilayani Lushoto Mkoani Tanga ambapo hapo kesho pamoja na maaskofu wengini ataongoza Ibada ya kuwekwa wakfu  Askofu Mteule wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu pamoja na kuingizwa kazini kwa msaidizi wa Askofu Mch .Michael Mlondakweli kanju.

Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Mhe.Januari Lugangika ametoa wito kwa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kupitia Dayosisi zake 26 kuweka kipaumbele kwenye agenda ya kukifufua Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (SEKOMU) kwani licha ya Chuo hicho kuwa na sifa ya kutoa taaluma bora na ya kipekee kimekuwa ni alama ya utume wa Kanisa kwa jamii.