Uncategorised
- Details

Askofu Dkt.Msafiri Joseph Mbilu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki leo tarehe 01/07/2021 ameshiriki kwenye Ibada ya ufunguzi wa mkutano mkuu (SINODI) KKKT Dayosisi ya Kaskazini Magharibi-Bukoba Jimbo la Kaskazini (A) Kigarama.Baba Askofu Dkt Msafiri Mbilu hapo kesho anatarajiwa kutoa mada kutoka kitabu cha Luka 14:28.Baba Askofu Dkt Msafiri Joseph Mbilu ndiye mnenaji mkuu katika mkutano huo.
- Details
Msaidizi wa Askofu KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Michael Mlondakweli Kanju ametoa pongezi kwa wafanyakazi wa vituo vya Nyumba ya masista (Nkwenda Mother House), Chuo cha Maarifa ya nyumbani Nkwenda,Shule ya msingi Tumshubire pamoja na Chuo cha Biblia Nkwenda kwa kazi nzuri wanayoifanya katika uendeshaji na utunzaji wa vituo hivyo

- Details

Tarehe 26/06/2021 imekuwa siku ya furaha katika Dayosisi yetu KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, ambapo katika Jimbo la Kusini tumekuwa na Ufunguzi wa Kanisa katika Usharika wa Msongolo mtaa wa Sinai.Katika ufunguzi huo Ibada iliongozwa na Baba Askofu Dkt Msafiri Joseph Mbilu .
- Details

Msaidizi wa Askofu KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki , Mch Michael Mlondakweli Kanju yupo ziarani KKKT Dayosisi ya Karagwe ambapo leo tarehe 25/06/2021 ameongoza ibada ya kufunga mwezi wa sita katika Kanisa Kuu la Lukajange .Akihubiri katika ibada hiyo kutoka kitabu cha Ufunuo wa Yohana 21:4 amesema kuwa kuna mahangaiko ya aina mbalimbali, machozi ya kila namna,maumivu pamoja na magonjwa,na hali ngumu ya maisha. Hii ni hali ya maisha ambayo watu wanapitia. Bwana Yesu anaahidi kwamba atafuta machozi haya na hayatakuwepo tena.
Page 109 of 125

