

Askofu Mteule wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch. Dkt Msafiri Joseph Mbilu pamoja na viongozi wengine wa Dayosisi wameshiriki Mazishi ya Baba mzazi wa Prof . Christopher Mahonge (Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa-SEKOMU) yaliyofanyika katika Kijiji cha Vuga, Lushoto leo tarehe 20/01/2021. Marehemu Mzee Paulo Mahonge enzi za uhai wake aliitumikia Lutheran Junior Seminary kwa miaka mingi.







