×

Warning

Failed deleting thumb_115_745.jpg

Naye atafuta kila chozi katika macho yao,wala mauti haitakuwepo tena,wala kilio,wala maumivu hayatakuwepo tena, kwa kuwa mambo ya kwanza , yamekwisha kupita UFUNUO 21:4.

Katibu Mkuu wa KKKT- Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch. Godfrey Tahona Walalaze kwa niaba ya uongozi wa KKKT- Dayosisi ya Kaskazini Mashariki anasikitika kutangaza kifo cha Mama. Damaris Appelesy Ketto,mama mzazi wa Mkuu wa Jimbo la Pwani, Mch Thadeus A. Ketto ,kilichotokea jana Ijumaa tarehe 14/01/2022.Ibada ya mazishi itafanyika siku ya Jumanne tarehe 18/01/2022 katika Kanisa la KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Usharika wa Mtonga - Korogwe. Uongozi unatoa pole kwa Mkuu wa Jimbo la Pwani, Mch. Thadeus A. Ketto, ndugu, jamaa na marafiki popote pale walipo. BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na libarikiwe