
Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu leo tarehe 20/01/2022 amekuwa na ziara ya kikazi katika Jimbo la Kusini na ameongoza kikao kazi kilicho jumuisha Wachungaji, Mashemasi pamoja na wainjilisti wa KKKT-DKMs Jimbo la Kusini pamoja na mambo mengine yaliyo jadiliwa katika kikao hicho kilichofanyika katika Usharika wa soni Baba Askofu amewakumbusha watumishi hao kuendelea kufanya kazi kwa uwazi na umakini mkubwa katika kila jambo wanalo lifanya.

Hata hivyo Baba Askofu Dkt Msafiri Mbilu katika kikao hicho ameeleza kufurahishwa kwake na matokeo mazuri ya kidato cha nne (Mwaka 2021) katika Shule za sekondari zinazo milikiwa na KKKT-DKMs na kuwapongeza walimu na wafanyakazi wote katika Shule hizo kwa kazi nzuri waliyoifanya na hivyo kutoa wito kwa wazazi na walezi kuwapeleka Watoto wao katika Shule hizo.

katika Shule ya Lwandai na Bangala Lutheran Junior Seminary matokeo ni kama inavyo onekana.



Msaidizi wa Askofu KKKT-DKMs, Mch. Michael Mlondakweli Kanju

Mkuu wa Jimbo la Kusini, Mch. Isai Mweta


