
Uongozi wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, unatoa pole kwa Baba Askofu Dkt. Fredrick Onael Shoo Mkuu wa KKKT na Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini,kufuatia kifo cha Askofu Mstaafu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini, Dkt. Erasto Kweka, kilichotokea tarehe:25/11/2023.
Uongozi unatoa pole kwa familia, Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Dayosisi ya Kaskazini ,Wakuu wa Majimbo wa Dayosisi ya Kaskazini, Wakuu wa Idara zote za Dayosisi Wachungaji wote wa Dayosisi ya Kaskazini pamoja na Washarika wote wa Dayosisi ya Kaskazini.
BWANA ametoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na libarikiwe.

Sehemu ya taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa KKKT- Dayosisi ya Kaskazini, Mhandisi Z.S. Moshi kwa,Wajumbe wa Halmashauri Kuu,Wakuu wa Majimbo, Wakuu wa Idara za Dayosisi Wachungaji wote wa Dayosisi ya Kaskazini, Washarika wote wa Dayosisi ya Kaskazini,INAELEZA:- Wapendwa, Nawasalimu katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo. Yah: TAARIFA YA TANZIA Mada husika hapo juu. Uongozi wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini, una masikitiko makubwa kutangaza kutwaliwa kwa Baba Askofu Mstaafu Dr. Erasto Kweka, kifo kimetokea leo tarehe 25 Novemba, 2023 saa nne asubui katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha moyo cha Jakaya Mrisho Kikwete. Baba Askofu Kweka amekuwa Kiongozi wa Dayosisi ya Kaskazini toka mwaka 1976-2004 alipostaafu. Uongozi wa Dayosisi utaendelea kuwajulisha mipango ya mazishi pale itakapokamilika.

