Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu anaendelea na ziara yake nchini Ujerumani, ambapo leo tarehe 06/03/2024 ametembelea Ofisi Kuu ya Kanisa la Kiinjili la Westphalia. Hili ni Kanisa lenye uhusiano Mkubwa na wa muda mrefu na Dayosisi yetu.
 
Hapa amepokelwa na mwenyeji wake Mch. Dkt. Albrecht Philips ambaye ni Mkuu wa Kurugenzi ya Uhusiano wa Kimataifa na Mission (Ecumenism, Mission and Global Responsibility) ambaye ataitembelea Dayosisi yetu mwezi Julai 2024.