Dayosisi yetu imepata heshima kubwa ya kushiriki katika Mkutano wa Kanda ya Afrika ulioandaliwa na United Evangelical Mission (UEM), uliofanyika katika mji wa Gaborone, nchini Botswana kuanzia tarehe 23 Februari hadi 1 Machi mwaka huu.

Katika mkutano huu muhimu dayosisi yetu  imewakilishwa na viongozi na wajumbe wafuatao:

  1. Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu

  2. Mch. Happiness Diu – Mjumbe wa Bodi ya UEM Afrika anayewakilisha wanawake

  3. Elvina Riziki – Mwakilishi kundi la  vijana

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, amefungua rasmi kikao cha tathmini kwa kazi zilizotekelezwa katika kipindi cha mwaka 2025.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho kilichofanyika tarehe 12/02/2026 katika Hoteli ya Tumaini Mbuyukenda, Jijini Tanga, Askofu Dkt. Mbilu amesema kuwa lengo kuu la kikao hicho ni kuweka msingi imara kwa watumishi kutambua walipotoka, walipo na wanakoelekea katika utendaji wao wa kazi. Amesisitiza kuwa tathmini ni nyenzo muhimu katika kupima mafanikio, kubaini changamoto na kupanga mikakati madhubuti ya kuboresha utendaji kwa siku zijazo.

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Dkt. Msafiri Mbilu, alipata fursa ya kupokea ugeni wa kiongozi wa undugu Helga Walter kutoka Hainberg-Gymnasium Göttingen  nchini Ujerumani. 

Katika mazungumzo yao yaliyofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki tarehe 05/02/2026  , pande zote mbili zilijadili kwa kina namna ya kuendelea kuimarisha na kuboresha undugu uliopo kati yao, hususani katika nyanja za elimu na huduma za kijamii.

Aidha, Askofu Dkt. Mbilu alitumia fursa hiyo kutoa shukrani za dhati kwa Helga pamoja na wadau wengine wa maendeleo kutoka Hainberg-Gymnasium Göttingen kwa michango yao ya kimaendeleo, hususani katika Shule ya Sekondari Lwandai pamoja na vituo vya diakonia vilivyopo Irente vinavyomilikiwa na KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki.

Ziara hiyo ilionesha mshikamano na dhamira ya pamoja ya kuendeleza ushirikiano wenye tija kwa manufaa ya jamii.

 

Kikao cha Kamati ya Utendaji ya Halmashauri Kuu ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania – Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMs) kilichofanyika  tarehe 29 Januari 2026 katika Ukumbi Mdogo wa Mikutano, Utondolo – Lushoto. Kikao hicho kimewakutanisha wajumbe wa Kamati ya Utendaji kwa ajili ya kujadili na kufanya maamuzi muhimu yanayohusu uendeshaji na maendeleo ya D