Uncategorised
- Details
Tarehe 19 Juni 1963, Kanisa la Usambara - Digo na makanisa mengine sita ya Kilutheri yaliungana na kuunda Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania . Leo hii KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMs) yenye Makao Makuu Wilayani Lushoto Mkoani Tanga ni miongoni mwa Dayosisi 28 za KKKT. Dayosisi inaitwa hivyo kwakuwa inapatikana Kaskazini Mashariki mwa Tanzania katika Mkoa wa Tanga. Kwahiyo KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMs) ni taasisi ya kidini iliyosajiliwa tarehe 19 Juni 1963 na Makao yake Makuu yapo Wilaya ya Lushoto Mkoa wa Tanga. Dhamira ya KKKT-DKMs ni kufundisha na kuhubiri neno la Mungu na kutoa huduma nzuri za kiroho, kimwili, kiakili, kiuchumi na kijamii kwa watu wote. Taasisi hii inatoa tangazo la kazi kwa nafasi moja ya MRATIBU WA HUDUMA YA MTOTO NA KIJANA kwa vijana wote (Wakristo)
NAFASI NA WAJIBU WA MRATIBU WA HUDUMA YA MTOTO NA KIJANA
- Details

Tarehe 19 Juni 1963, Kanisa la Usambara - Digo na makanisa mengine sita ya Kilutheri yaliungana na kuunda Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania . Leo hii KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMs) yenye Makao Makuu Wilayani Lushoto Mkoani Tanga ni miongoni mwa Dayosisi 28 za KKKT. Dayosisi inaitwa hivyo kwakuwa inapatikana Kaskazini Mashariki mwa Tanzania katika Mkoa wa Tanga. Kwahiyo KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMs) ni taasisi ya kidini iliyosajiliwa tarehe 19 Juni 1963 na Makao yake Makuu yapo Wilaya ya Lushoto Mkoa wa Tanga. Dhamira ya KKKT-DKMs ni kufundisha na kuhubiri neno la Mungu na kutoa huduma nzuri za kiroho, kimwili, kiakili, kiuchumi na kijamii kwa watu wote. Taasisi hii KUPITIA COMPASSION inatangaza nafasi moja ya kazi ya Mtendakazi wa Huduma ya Kunusuru Maisha ya Mama na Mtoto.
SIFA ZA MTENDAKAZI WA HUDUMA YA KUNUSURU MAISHA YA MAMA NA MTOTO
NAFASI: Mtenda kazi katika Huduma ya Kunusuru Maisha ya mama na mtoto (HBI).
MAHALI: Kituo cha huduma ya mtoto na kijana.
KUWAJIIBIKA: Atawajibika kwa Mratibu wa kituo cha huduma ya maendeleo ya mtoto na kijana.
Muhtasari wa majukumu ya kazi kwa mtendakazi
Mtendakazi wa huduma ya afua ya kunusuru maisha ya mama na mtoto kwa huduma za nyumbani (Survival & Sponsorship Home Based) atahusika moja kwa moja na akina mama na watoto watakaonufaika na huduma hii. Atatumia asilimia 80% ya muda wake wa kazi kwa kuwatembelea akina mama hao nyumbani kwao na kutoa mafunzo kwa kutumia mitaala mbalimbali ya afua hii. Yeye ndiye atawajibika kutekeleza afua akishirikiana na watendakazi wengine katika kuhakikisha masuala yote katika program ya afua ya mama na mtoto yanatekelezwa. Ni jukumu la mtendakazi kufuatilia mwenendo wa namna malengo ya afua ya mama na mtoto yatakavyosababisha tofauti kwa walengwa katika maisha ya kila siku Mtendakazi atafuatilia na kuhakikisha upimaji wa ukuaji wa mtoto unafanyika kila mwezi kwa utaratibu uliowekwa na kuingiza taarifa kwenye mfumo wa mawasiliano wa Connect. Awe ni mfano wa kuigwa katika ukristo wake, anayeheshimu watu na mwenye kutunza siri za watu.
- Details
MAKAYO KOROGWE: Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania - Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMs) amewataka Wakristo kuacha kufuata mafundisho potofu na badala yake wachukue jukumu la kuyashuhudia Maandiko Matakatifu kwa wengine.

Akizungumza Alhamisi, Julai 31, 2025, wakati wa Ibada ya Kipaimara iliyofanyika katika Jimbo la Magharibi, Usharika Mteule wa Msomera, Mtaa wa Makayo, Askofu Dkt. Mbilu alisisitiza kuwa ni wajibu wa kila mmoja kushuhudia nuru ya kweli na upendo wa Yesu Kristo.

Askofu Dkt. Mbilu amewataka washarika wa Mtaa wa Makayo, ambao wengi wao ni jamii ya wafugaji wa Kimasai, kuacha kuwasikiliza watu wanaokwenda maeneo yao na kudai kuleta "nuru ya Wamasai," akisisitiza kuwa Yesu anatosha na yeye ndiye Nuru ya Ulimwengu. Aliwahimiza kuiga mfano wa Yesu Kristo, ambaye aliupenda ulimwengu wote na hakuja kwa ajili ya Wamasai pekee bali kwa ajili ya ulimwengu mzima.
Katika Ibada hiyo ilitanguliwa na ufunguzi wa Kanisa la Usharika Mteule wa Msomera, Mtaa wa Makayo. Jumla ya vijana 64 walibarikiwa na walichangia Tsh. 310,000 na mara baada ya kuungwa mkono na wanaume na wanawake waliohudhuria Ibada hiyo, jumla ya shilingi 585,000 zilipatikana na zitaelekezwa katika ulipaji wa deni la Dayosisi.
Tufuatilie kwenye mitandao yetu ya kijamii
Page 7 of 125


