Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amewasihi wahasibu na watunzahazina wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki kuwa waaminifu katika utendaji wao wa kazi na kuimarisha mifumo mbalimbali ya fedha ili kuwezesha uhifadhi wa taarifa za fedha kwa ufasaha zaidi.
 
Askofu Dkt. Mbilu ameyasema hayo leo tarehe 14/03/2023 kwenye ufunguzi wa mafunzo yanayowakutanisha wahasibu na watunza hazina. Mafunzo haya yanalenga kuwajengea uwezo na uelewa juu ya mifumo ya kifedha pamoja na kuwa na mfumo mmoja wa kifedha wa Dayosisi.
Mafunzo hayo yanaratibiwa na Mkurugenzi wa fedha na Utawala wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki CPA.  Peter John Singano. Mafunzo hayo yanayofanyika katika Taasisi ya ELIMU ya Kolowa Technical Training Institute (KOTETI ) iliyopo Magamba Lushoto nayameanza leo tarehe 14/03/2023 na yatamalizika tarehe 16/03/2023 .