Siku ya leo tarehe 27/09/2025 wakiambatana na mwenyeji wao Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Dkt.Msafiri Joseph Mbilu pamaoja na maafisa wengine wa Ofisi Kuu ya KKKT-DKMs, wageni hawa wametembelea Chuo cha Kolowa Technical Training Institute (KOTETI), Makazi ya Askofu, Makao Makuu ya KKKT-DKMs,Eneo la Vibanda vya Biashara vinavyo milikiwa na KKKT-DKMs, Irente Rainbow School, Irente Children Home pamoja na Shule ya Wasioona Irente.