Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amempongeza Mch. Happiness Diu kwa kuchaguliwa kwenye Mkutano Mkuu wa UEM Afrika kuwa mjumbe wa Bodi ya UEM kwa kanda ya Afrika nzima.
Askofu Dkt. Mbilu ameongeza kuwa ni jambo la kujivunia kwa KKKT-DKMS kupata muwakilishi katika nafasi hiyo kubwa kwenye uongozi wa UEM kwa Bara la Afrika.
Mkutano huo uliofanyika Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa Luther House KKKT-Dayosisi ya Mashariki na Pwani ulianza tarehe 21/03/2023 na utafungwa hivi leo tarehe 25/03/2023.
Kwenye Mkutano huo kutoka KKKT-DKMS umehudhuria na wajumbe watatu ambao ni Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, Mch. Happiness Diu akiwakilisha Wanawake na Mwl. Nora Kimaro ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Vijana KKKT-DKMS akiwakilisha Vijana.
UEM: United Evangelical Mission ni chama Cha kiinjili Cha kimisioni kilianzishwa mwaka 1996 na wamisionari kutoka Ujerumani wa Rhenish na Betheli ambao walifika Africa, na Asia kwa ajili ya kuanzisha shughuli za Dini. Katika Africa walifika katika nchi 7 ambazo ni Tanzania, DR Congo, Africa ya Kusini, Botswana, Cameroon, Namibia na Rwanda kukiwa na madhehebu 15. Katika Tanzania inawakilishwa na Makanisa 4 ya KKKT ambayo ni KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, KKKT Dayosisi ya Kaskazini Magharibi, KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani pamoja na KKKT Dayosisi ya Karagwe.