
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Inatangaza Nafasi moja ya Kazi ya KATIBU WA AFYA WA DAYOSISI.
MAJUKUMU YA KAZI INAYOOMBWA NI PAMOJA NA:
- Kutayarisha Mipango na Makisio ya fedha za shughuli zinazohusiana na Afya
- Kutayarisha Taarifa za Shughuli za uendeshaji na Utekelezaji za Mwezi,Robo mwaka na Mwaka mzima.
- Kusimamia matumizi ya Fedha na ununuzi wa Vifaa kama ilivyo katika miongozo ya fedha na ununuzi.
- Kusimamia na kutathimini utendaji wa kazi wa Watumishi kulingana na taratibu zilizokubalika.
- Kuandaa Mipango ya Usafiri kwa Wagonjwa
- Kutoa ushauri wa Kiutawala katika masuala ya kila siku kuhusu utekelezaji wa shughuli za Afya.
- Kufundisha watumishi utunzaji wa rasilimali za Afya (Watumishi,fedha,vifaa na muda)
- Kusimamia na kutathimini uendeshaji shughuli za Afya.
- Kuitisha Vikao mbalimbali pamoja na kuandika mihutsari ya Vikao hivyo vya kiutendaji.
SIFA ZA MUOMBAJI
- Mwenye Elimu ya Kidato cha 4 au 6 na aliehitimu mafunzo ya shahada ya Kwanza ya Menejimenti ya Afya (Health System Management katika Chuo kinachotambulika na Serikali ya Tanzania.
- Awe Mtanzania na mwenye umri usiozidi miaka 45.
- Uzoefu wa Kazi sio chini ya Miaka 2.
- Maombi yote yaambatanishwe na Nakala ya Vyeti vya taaluma na vya Kidato cha 4 au cha 6 pamoja na cheti cha kuzaliwa.
- Waombaji waambatanishe maelezo yao binafsi yaliojitosheleza na yenye anuani zao na namba zote za simu, Na picha 2 za passport za hivi karibuni ya muombaji
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 06/11/2021 Saa tisa na nusu (09:30) Alasiri, Maombi yote yatumwe kwa Ofisi ya Katibu Mkuu-KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki S.L.P 10 LUSHOTO Barua Pepe This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

