Naye atafuta kila chozi katika macho yao,wala mauti haitakuwepo tena,wala kilio,wala maumivu hayatakuwepo tena, kwa kuwa mambo ya kwanza , yamekwisha kupita UFUNUO 21:4.

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Mashariki na Pwani (DMP) Mch. Dkt. Alex G. Malasusa, Leo tarehe 08/10/2021 ameongoza Ibada ya mazishi ya marehemu Mchungaji Mstaafu Elihudi  Efrahimu Sekumbo,

akishirikiana na msaidizi wa Askofu KKKT-DKMs Mch Michael Mlondakweli Kanju, katika Usharika wa Hengiti Mtaa wa Mbaru (KKKT-DKMs).

Mchungaji Mstaafu Elihudi Sekumbo ambaye kwa sehemu kubwa katika utumishi wake alitumika katika Dayosisi ya Mashariki na Pwani(DMP) alizaliwa tarehe 24/12/1939 wilayani Lushoto Mkoa wa Tanga.

Marehemu Mch Elihudi Sekumbo alianza utumishi katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Mashariki na Pwani mnamo mwaka 1986 hadi mwaka 1993 akiwa Mwinjilisti na mwaka 1993 alibarikiwa kuwa Mchungaji.

Marehemu Mch. Mstaafu Elihudi Sekumbo aliitwa na Bwana usiku wa tarehe 04/10/2021 akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako alikuwa anapatiwa matibabu.

Kwa niaba ya Uongozi wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini kupitia Msaidizi wa Askofu Mch. Michael Mlondakweli Kanju ambaye alimuwakilisha Askofu Mch.Dkt Msafiri Mbilu kwenye Ibada hiyo ya mazishi amesema kuwa, Uongozi unapenda kutoa pole kwa Familia ya Marehemu, watumishi wote wa KKKT-Dayosisi ya Mashariki na Pwani, ndugu jamaa na marafiki walioguswa na msiba huu mzito. Mungu awape nguvu na Faraja ya kweli katika kipindi hiki kigumu.

Sharika ambazo Marehemu Mchungaji  Mstaafu Eliudi Sekumbo alitumika akiwa Mwinjilisti ni 

  • Usharika wa Kunduchi
  • Usharika wa Wazohill
  • Usharika wa Ukonga
  • Usharika wa Temeke Wiles
  • Usharika wa Tumbi
  • Usharika wa Soga
  • Usharika wa Magogoni

Sharika ambazo Marehemu Mchungaji  Mstaafu Eliudi Sekumbo alitumika akiwa Mchungaji ni

  • Usharika wa Mabibo External 
  • Usharika wa Maneromango
  • Usharika wa Kimanga
  • Usharika wa Mburahati
  • Usharika wa Hananasifu
  • Usharika wa Pugu Kajiungeni
  • Usharika wa Kipunguni B
  • Usharika wa Pugu Sekondari.