Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch. Dkt Msafiri Joseph Mbilu amefungua Kongamano la Maombi Kanda ya Kaskazini ikijumuisha Mikoa ya Manyara,Arusha Kilimanjaro na Tanga linaloongozwa na Mwl Christopher Mwakasege na kusema kuwa ni baraka kwa Taifa na kanda ya Kaskazini kupata kibali kutoka kwa Mungu kwakuwa sehemu ya kuliombea Kanisa,Taifa pamoja na viongozi wake.
Askofu Dkt. Mbilu ameyasema hayo akizindua kongamano hilo tarehe 22/03/2024 katika Ukumbi wa Mikutano wa Benjamin William Mkapa Auditorium uliopo katika, Chuo cha Kolowa Technical Training Institute (KOTETI) kilichopo Magamba Wilayani Lushoto Mkoani Tanga nakuwasisitiza waombaji hao kuwa mstari wa mbele katika kupinga maovu na yale yote yasiyo mpendeza Mungu.
Kwa upande wake Mwalimu wa Neno la Mungu Mwl Christopher Mwakasege amempongeza Askofu Dkt. Mbilu kwa kuwa na maono,utayali wa kulipokea kongamano hilo Wilayani Lushoto na kusema ni muhimu kuwekeza kwenye maombi kwaajili ya Taifa na hivyo kuwapongeza washiriki wote waliohudhuria kongamano hilo kwakuwa kwakufika kwao wamewekeza kwa Mungu.
 
Kwa upande wa Waratibu na Washiriki wa Kongamano hilo akiwemo Mwalimu Christina Peter pamoja na Mwinjilisti Mwivano Shelukindo wamesema kuwa kongamano hilo limekuwa la baraka kwani litawapa nafasi ya pamoja kama waombaji kuliombea Taifa na Viongozi wake sambamba na kuliombea Kanisa kwakuwa Mungu ni yote katika yote.
Pamoja na hayo Mwl. Christopher Mwakasege akiambatana na baadhi ya wajumbe wa huduma ya MANA, amepata wasaa wa kutembelea Makao Makuu ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki na kupokelewa na mwenyeji wake Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu ambapo mara baada ya mazungumzo yao Mwl. Mwakasege alifanya maombi pamoja na Watumishi wa Ofisi Kuu.