Dean Mteule Frank Richard Mntangi, ametambulishwa rasmi katika Makao Makuu ya Ofisi ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMs) yaliyopo Lushoto Tanga. Zoezi hili la utambulisho lililoongozwa na Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu. Dean Mtangi amepokelewa na kutambulishwa kwa wakurugenzi pamoja na watumishi wa Ofisi Kuu.
Dean Mteule Mntangi, akizungumza kwenye Ibada ya asubuhi ya leo tarehe 15/04/2025 ameahidi kutumika kwa uaminifu katika nafasi hiyo na kuahidi kutoa ushirikiano katika idara,vitengo na watenda kazi wote katika Dayosisi ili kufikia malengo,maono na mipango ya Dayosisi.
Kwa upande wake Dean Mstaafu Kanju amemshukuru Askofu Dkt. Mbilu, kwa kumuamini kwa miaka yote aliyokua msaidizi wake kuanzia tarehe 01/12/2020,ametoa shukrani za dhati kwa kurugenzi na watumishi wote wa Ofisi Kuu kwa jinsi walivyomuonyesha ushirikiano,upendo na mshikamano katika kipindi chote cha utumishi wake katika Ofisi ya Msaidizi wa Askofu.
Makabithiano ya ofisi yameanza kufanyika leo tarehe 15/04/2025 na ya taendelea mpaka siku za usoni kutokana na ukubwa na umuhimu wa Kurugenzi ya Misioni na Uinjilisti kama kurugenzi mama katika Dayosisi.
Dean Mteule Mch. Mntangi ataingizwa kazini rasmi tarehe 20/07/2025 katika Usharika wa Kanisa Kuu Lushoto.