Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania  Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Inatangaza Nafasi  moja ya Kazi ya KATIBU WA AFYA WA DAYOSISI.

Askofu wa KKKT- Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch. Dkt. Msafiri Joseph Mbilu leo tarehe 26/09/2021, amejumuika na Washarika wa Usharika wa Bumbuli Jimbo la Kusini katika Ibada ya Jumapili, Ibada hiyo ilikuwa na matukio mbalimbali.

 Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch. Dkt. Msafiri Joseph Mbilu leo tarehe 19/09/2021 ameongoza Ibada ya Jumapili katika Usharika wa Soni Mtaa wa Kwangwenda, Ibada hii ilikuwa na tukio la Uwekwaji wa jiwe la msingi la kanisa  pamoja na harambee ya ujenzi wa Kanisa la mtaa wa kwang’wenda.

Katika harambee hio Jumla ya  shilingi milioni kumi na moja hamsini na moja elfu na miatano hamsini (11,051,550)  ilipatikana kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa hilo lililowekewa jiwe la msingi.