×

Warning

Failed deleting thumb_115_745.jpg

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch. Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amewapongeza wachunguji walio barikiwa mnamo tarehe 30,06,1991 na kuingia katika hudumu ya kichungaji tayari kutumika shambani mwa Bwana.

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch.Dkt.Msafiri Joseph Mbilu amekutana na kufanya mazungumzo na Mch.Dkt.Ulrich Mouller (Vice moderator UEM) ambaye aliambatana na Mch.Dkt. Ernest Kadiva (The deputy Executive secretary in Africa) Leo tarehe 14/08/2021 alipo tembelea makao makuu ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki.

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu leo tarehe 08/08/2021 ameongoza Ibada ya Jumapili katika Usharika wa Mombo mtaa wa Buiko.

Kaimu katibu Mkuu wa KKKT- Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch. Godfrey Tahona Walalaze kwa niaba ya uongozi wa KKKT- Dayosisi ya Kaskazini Mashariki  anasikitika kutangaza kifo cha mke wa marehemu Mch. Yohana  Nyaki, Mama Makinyemi Y. Nyaki kilichotokea leo tarehe 30/07/2021 nyumbani kwao Fuizai, mazishi yatafanyika siku ya kesho mchana  tarehe 31/07/2021 na Ibada ya mazishi itafanyika  katika Usharika wa Fuizai .

Uongozi unatoa pole kwa familia ya marehemu Mch.Yohana  Nyaki, ndugu, jamaa na marafiki popote pale walipo. BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na libarikiwe.