Uncategorised
- Details

Picha rasmi ya Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu ,wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, nakala halisi iliyochapishwa Inapatika Makao Makuu ya KKKT-DKMs. Kwa mawasiliana wasiliana nasi kupitia This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. au 0764105944/0655449481
Picha hii ndio itatumika katika Ofisi zote za Sharika za KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki
- Details

Leo tarehe 12/09/2021 imekuwa siku ya baraka kwa washarika wa Usharika wa Kisosora Jimbo la Pwani. Ambapo imefanyika Ibada iliyokuwa na matukio mbalimbali vijana wapatao 19 wamepata kipaimara na wawili kati yao walibatizwa.
- Details

Uongozi wa Shule ya Seminari ndogo ya Bangala iliyopo Halmashauri ya Bumbuli Vuga inawatangazia nafasi za kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka wa masomo 2022 kwa vijana waliomaliza darasa la saba mwaka huu 2021, mtihani wa kujiunga utafanyika tarehe 11/09/2021 na tarehe 25/09/2021. fomu za kujiunga zinapatikana katika vituo vifuatavyo.
Shuleni Bangala,Tumaini Bookshoop(Lushoto),Korogwe , Muheza, Handeni, Makorora, Kana.Pia tuna nafasi chache za wanaopenda kuhamia katika shule yetu kwa kidato cha tatu.
- Details

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch. Dkt. Msafiri Joseph Mbilu leo tarehe 30/08/2021 amefanya ziara ya kikazi katika Shule ya Sekondari Lwandai. Katika ziara hiyo Baba Askofu Mbilu alitembelea mazingira ya Shule na kupokea taarifa iliyowasilishwa na Mkuu wa Shule hiyo, Mch. Daniel Mwarabu na waandamizi wa idara mbalimbali za shule hiyo.
Page 104 of 125

