Askofu Dkt Msafiri Joseph Mbilu, leo tarehe 23/05/2021 ametembelea na kuonana na wanafunzi,walimu pamoja na wafanyakazi wa Shule ya Sekondari  Lwandai inayo milikiwa na KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki kwa lengo la kuwasalimu.

 

 

Askofu Dkt Msafiri Joseph Mbilu akiwasili Mlalo kwenye Ibada ya KUINGIZWA KAZINI Mkuu wa Jimbo la Kaskazini Mch. Andeson Moses Kipande.

Mahubiri ya Baba Akofu Dkt Msafiri Joseph Mbilu Leo tarehe 16/05/2021

Ndugu zangu wapendwa katika Bwana. Siku hii ya leo tumeamua iwe siku ya KANTATE DOMINO kutokana na maandalizi yatu ya siku zilizopita. Kimsingi siku hii ni ya kusubiri ahadi ya Baba kutupa Roho Mtakatifu baada ya kupaa kwa Bwana. Lakini tendo lenyewe la uimbaji linaongozwa na huyo Roho wa Mungu pia. Kuimba ni kipawa kutoka kwa Mungu mwenyewe.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa pamoja na Maaskofu wapatao 18 wameshiriki katika Ibada ya kuwekwa wakfu na Kusimikwa kazini Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mchungaji Dkt. Msafiri Joseph Mbilu.Waziri Mkuu ameshiriki Ibada hiyo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.