Askofu Mteule wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch. Dkt. Msafiri Joseph Mbilu pamoja na viongozi wengine wa Dayosisi watatembelea Dayosisi ya Mashariki na Pwani (DMP) tarehe 28/03/2021 ambapo watashiriki na kuongoza Ibada katika baadhi ya sharika za DMP.

Askofu Mteule wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amesaini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga leo tarehe 22 Machi 2021.