Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, amewapongeza Wanawake wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki hususani Wanawake wa Usharika wa Irente kwa mambo makubwa wanayoendelea kuyafanya katika Dayosisi.
Wanawake hao wamepongezwa kutokana na kuuenzi mwaka wa Wanawake na kuwataka kuendelea kufanya hivyo ili mwaka wao ujioneshe na kujitambulisha wenyewe kwa kazi mbalimbali wanazozifanya na watakazoendelea kuzifanya.

MATUKIO KATIKA PICHA: Ibada ya uwekwaji wa Jiwe la Msingi la Kanisa katika Jimbo la Pwani,Usharika Mteule wa Ng’ambo ya Mto Pangani-Sange iliyoongozwa na Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu leo tarehe 17/11/2022.

Pamoja na uwekwaji wa jiwe la Msingi pia wameingizwa kazini Wazee wa Kanisa na viongozi wa kamati mbalimbali.

KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki mnamo tarehe 15/11/2022 ilipokea ugeni kutoka KKKT-Dayosisi ya Ulanga Kilombero kwa lengo la kujifunza na kudumisha undugu kati ya Dayosisi hizi mbili.

Leo tarehe 12/11/2022 imekuwa siku ya furaha na baraka tele kwa Washarika wa Usharika wa Malindi Mtaa wa Kana Mpya ambapo Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu ameongoza Ibada iliyokuwa na tendo la uwekwaji wa Jiwe la Msingi na ufunguzi wa Kanisa.



KATIKA HISTORIA:- Ibada katika Mtaa huu wa Kana Mpya, zilianza rasmi mwaka 2012 nyumbani kwa mzee Shabani Vuri kwa miaka mitatu mnamo mwaka 2015 Usharika ulipata eneo ambalo ndipo lilipojengwa Kanisa lililo funguliwa leo.