KANISA LA KIINJILI LA KILUTHERI TANZANIA

DAYOSISI YA KASKAZINI MASHARIKI

S.L.P. 10 (SIMU 027 – 2660027 / FAX 027 -2660092) LUSHOTO

E-mail: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

UUZAJI WA MBAO ZA MIKARATUSI KATIKA SHAMBA LA KKKT -DKMs IRENTE-LUSHOTO

1) Kanisa la Kiinjili la Kiluteri Tanzania-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMs) itauza mbao aina ya Mikaratusi yenye jumla ya meta za ujazo 944.28 zilizopo katika shamba la Irente Wilaya ya Lushoto. Mbao hizo zitauzwa huko Irente mahali zilipo na hivyo wanunuzi wanaalikwa kufika huko.

2) Wanunuzi wanakaribishwa kutembelea shamba sehemu zilipo mbao tajwa wakati wa saa za kazi kuanzia saa tatu (3:00) asubuhi hadi saa tisa (9:00) alasiri siku za Jumatatu hadi Jumamosi. Meneja wa shamba husika au wasaidizi wake watakuwepo kwa ajili ya mauzo na pia kutoa maelezo ya ziada.

"Matengenezo ya Kanisa si jambo la kutokea kwa mara moja hivyo Kanisa linapaswa kuwa katika hali ya matengenezo wakati wote kwa kuisikiliza sauti ya Roho Mtakatifu" Askofu Dkt. Fredrick Shoo, Mkuu wa KKKT.

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini  Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu ameonyesha kuridhishwa na hali na mwenendo mzuri wa Shule ya Sekondari ya Lwandai na kuwapongezi walimu na wafanyakazi wa Shule hiyo kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kurejesha heshima ya Shule hiyo kongwe hapa Nchini.

 

MKUU WA KKKT BABA ASKOFU DKT. FREDRICK ONAEL SHOO.

Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Fredrick Shoo leo tarehe 18/10/2022, amefungua mafunzo ya siku mbili yanayohusu utoaji wa huduma bora za Afya katika Hospitali na vituo vya Afya vinavyo milikiwa na  KKKT.

Mafunzo haya yanafanyika  Jijini Dodoma ambapo  yamehudhuriwa na wajumbe kutoka Hospitali 23 na vituo vya Afya 24 vya KKKT. Wajumbe hao ni pamoja na maaskofu, makatibu wakuu pamoja na wataalamu wa Afya.