Uncategorised
- Details
\
Sehemu ya Wajumbe wengine wa Kamati ya Uhusiano
PICHA YA PAMOJA mara baada ya mazungumzo ya Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu na Mkuu wa Jimbo la Vlotho Mch. Dorothea Goudefroy (wa pili kutoka kushoto) pamoja na wajumbe wa kamati ya Undugu toka Vlotho.
- Details
Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu yupo ziarani Nchini Ujerumani yenye lengo la kuimarisha urafiki na amepata wasaa wa kutoa taarifa mbalimbali juu ya urafiki na hali ya Dayosisi kwa sasa katika sharika na vituo mbalimbali. Ziara hii ya Baba Askofu Dkt. Mbilu nchini Ujerumani inatoa fursa ya kukuza uhusiano na urafiki wa kihistoria kati ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki pamoja na marafiki waliopo nchini humo wenye urafiki na Sharika na Vituo vya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki.

"Askofu Mbilu. nimekuwa na mazungumzo ya moja kwa moja na marafiki zetu na baada ya hapo niliingia kwenye mazungumzo rasmi na kujikita zaidi katika kutafuta namna ya kuimarisha ushirikiano uliopo na mahusiano kati yetu na marafiki zetu waliopo hapa Ujerumani"-Askofu Dkt. Mbilu.
- Details

Leo tarehe 18/09/2022 Imekuwa siku ya baraka tele kwa washarika wa Usharika wa Malibwi Jimbo la Kaskazini ambapo vijana wa Kipaimara wapatao 106 walibarikiwa na wa 3 kati yao walibatizwa, Ibada iliongozwa na Msaidizi wa Askofu KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch. Michael Mlondakweli Kanju katika

Ibada iliyohudhuriwa na Wachungaji, Wainjilisti, Kwaya, Washarika pamoja na watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya Usharika wa Malibwi.

MKUU WA JIMBO LA KASKAZINI MCH: ANDERSON KIPANDE.

Awali kabla ya Ibada hiyo Msaidizi wa Askofu Mch. Michael Kanju alizindua mnara wa Kengere na nyumba ya mtumishi katika Usharika huo wa Malibwi Mtaa wa Kwedeghe.

Msaidizi wa Askofu Mch. Michaele Kanju katika matukio hayo, amemuwakilisha Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu ambaye yupo Nchini Ujerumani kwa ziara ya kikazi.
Aidha kufuatia kuitwa mbinguni kwa Baba Mzazi wa Shemasi Rehema Mbura Mzee Solomoni Baraza Msaidizi wa Askofu Mch. Michael Kanju amefika na kutoa pole kwa familia ya Marehemu Mzee Solomoni Baraza .


Marehemu Mzee Solomoni Baraza aliitwa mbinguni tarehe 15/09/2022 na mwili wake utapumzishwa katika makaburi yaliyopo katika Mtaa wa Mshangai Mission Jumanne ya tarehe 20/09/2022.
Ufunuo 14:13 “Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao”.
Uongozi wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, unatoa pole katika kipindi hiki kigumu kwa familia ya Marehemu Mzee Solomoni Baraza, ndugu, jamaa na marafiki popote pale walipo. BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na lihimidiwe.
- Details

“lichungeni kundi la Mungu lililo kwenu, na kulisimamia, si kwa kulazimishwa, bali kwa hiari kama Mungu atakavyo; si kwa kutaka fedha ya aibu, bali kwa moyo.”
— 1 Petro 5:2
Page 70 of 124

