Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt.  Msafiri Joseph Mbilu kama msimamizi wa mali za Dayosisi kupitia halmashauri Kuu ambayo yeye ni mwenyekiti wake amesema kuwa watahakikisha majibu ya zilipo fedha za utekelezaji wa miradi mbalimbali ndani ya Dayosisi ambazo hazikutumika kama ilivyokusudiwa yanapatikana.

Katika kufanikisha hilo amesema kuwa watumishi mbalimbali ikiwemo wachungaji waliokuwa wakiwajibika kusimamia fedha hizo wataulizwa hata ikibidi kwa ukali.

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, leo tarehe 21 Novemba, 2021 ameongoza Ibada ya Kipaimara katika Usharika wa Mgwashwi, Jimbo la Kusini.

Imekuwa siku ya furaha na baraka tele kwa washarika wa Usharika wa Mgwashwi ambapo jumla ya vijana wapatao 140 walibarikiwa na wawili kati yao walibatizwa.

Baba Askofu Dkt. Msafiri Mbilu amewakumbusha vijana hao walio barikiwa kutokuondoka katika kweli ya neno la Mungu  na kamwe wasiyumbishwe na mafundisho potofu ya neno la Mungu yaliyo kisiri katika nyakati hizi.

Msaidizi wa Askofu KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch. Michael Mlondakweli Kanju ameupongeza uongozi wa kituo cha Redio Utume Fm  chini ya Kaimu  meneja wa kituo hicho Bi. Evelyne Balozi Mariki kwa kuendeleza  maono ya Dayosisi ya kueneza Injili kwa wote.

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amekutana na kufanya mazungumzo na Mratibu wa Mawasiliano wa KKKT, ndugu Erick Adolph ambae ametembelea Makao Makuu ya KKKT-DKMs leo tarehe 19 Novemba, 2021.