Leo tarehe 31/10/2021 imekuwa siku ya baraka kwa washarika wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Usharika wa Irente Jimbo la Kusini ambapo vijana wapatao 24 walipata kipaimara. 

Leo tarehe 30/10/2021 Imekuwa siku ya baraka tele kwa washarika wa Usharika wa Hale Jimbo la Tambarare kwani vijana wapatao 164 walipata kipaimara na sita 6 kati yao walibatizwa.

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Mashariki na Pwani Mch Dkt. Alex Malasusa amewakumbusha waimbaji kuwa uimbaji unamchango mkukwa katika kumuita mtu kwa mungu na uimbaji umetumika kama chombo cha uinjilisti hivyo kukuwa kwa injili katika KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki na sehemu nyingine upo mchango mkubwa wa waimbaji.

Ikiwa ni mara ya kwanza tangu Kuchaguliwa na Kuingizwa kazini kuiongoza KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amewashukuru washarika wa Usharika wa Mkata kwa namna wanavyoendelea kumtumikia Mungu.