SIKU YA BWANA YA 4 BAADA YA PASAKA
JUMAPILI YA TAR. 15 MEI, 2022
NENO KUU:
"MWIMBIENI BWANA WIMBO MPYA" (KANTATE DOMINO)
"Kila mwenye pumzi na Amsifu Bwana"
ZAB.147:7--11
7 Mwimbieni Bwana kwa kushukuru, Mwimbieni Mungu wetu kwa kinubi.8 Huzifunika mbingu kwa mawingu, Huitengenezea nchi mvua, Na kuyameesha majani milimani.9 Humpa mnyama chakula chake, Wana-kunguru waliao.10 Hapendezwi na nguvu za farasi, Wala hairidhii miguu ya mtu.11 Bwana huwaridhia wao wamchao, Na kuzitarajia fadhili zake.
SIKU YA BWANA YA NNE INAYOFUATA PASAKA
Mwimbieni Bwana wimbo mpya (Kantate Domino)
AYA YA SIKU
"Mwimbieni Bwana wimbo mpya, kwa maana ametenda mambo ya ajabu" Zab.98:1
SALA
Mwenyezi Mungu, wewe peke yako waweza kuzitawala nia za waaminio kwa umoja; Uwajalie watu wako kupenda uliyoyaamuru na kutaka uliyoyaahidi, ili katika dunia hii isiyo na raha, mioyo yetu istarehe huko kwenye furaha ya kweli. Kwa Yesu Kristo, Mwana wako na Bwana wetu. Amen.
SOMO LA 1: 2 The. 2:13--17
13 Lakini imetupasa sisi kumshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu, ndugu mliopendwa na Bwana, kwa kuwa Mungu amewachagua tangu mwanzo mpate wokovu, katika kutakaswa na Roho, na kuiamini kweli;14aliyowaitia ninyi kwa injili yetu, ili kuupata utukufu wa Bwana wetu Yesu Kristo.15 Basi, ndugu, simameni imara, mkayashike mapokeo mliyofundishwa, ama kwa maneno, ama kwa waraka wetu.16 Na Bwana wetu Yesu Kristo mwenyewe, na Mungu Baba yetu, aliyetupenda akatupa faraja ya milele na tumaini jema, katika neema, 17awafariji mioyo yenu, na kuwafanya imara katika kila neno na tendo jema.
SOMO LA 2 MAHUBIRI:
Zab.104:33--35
33Nitamwimbia Bwana maadamu ninaishi; Nitamshangilia Mungu wangu nikiwa hai;34 Kutafakari kwangu na kuwe kutamu kwake; Mimi nitamfurahia Bwana. 35 Wenye dhambi waangamizwe katika nchi, Watendao ubaya wasiwepo tena. Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana.

