Uncategorised
- Details

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu akisaini kitabu cha maombolezo.
Naye atafuta kila chozi katika macho yao,wala mauti haitakuwepo tena,wala kilio,wala maumivu hayatakuwepo tena, kwa kuwa mambo ya kwanza , yamekwisha kupita UFUNUO 21:4.

- Details
KATIKA PICHA: Ufunguzi wa Tawi la Benki ya CRDB Wilayani Lushoto uliofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Omary Tebweta Mgumba leo tarehe 29/08/2022. Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu alishiriki katika ufunguzi huo.Tawi hilo la Bank ya CRDB lipo katika jengo linalomilikiwa na KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki.
MKUU WA MKOA WA TANGA MHE. OMARY TEBWETA MGUMBA akikata utepe kuashiria kufunguliwa rasmi kwa Tawi la CRDB Lushoto.
Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, akitoa salamu za Dayosisi na kufungua kwa maombi shughuli za ufunguzi wa Tawi la Benki ya CRDB Lushoto.
- Details
KATIKA PICHA: Ibada ya Jumapili ya leo tarehe 28/08/2022 iliyofanyika katika Usharika wa Kisosora Jimbo la Pwani na kuongozwa na Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu.Ibada hiyo ilkuwa na tendo la kuwabariki vijana wa kipaimara kumi na moja (11) na wawili (2) kati yao walibatizwa.

Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu akimbariki mmoja wa vijana waliopokea Kipaimara.
- Details
Katibu Mtendaji Fedha na Utawala wa UEM ndugu Timo Pauler amekutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki.Ambapo pia alipata nafasi ya kutembelea baadhi ya Sharika na Vituo ndani ya Jimbo la Pwani.
Katibu Mtendaji Fedha na Utawala wa UEM Ndugu Timo Pauler, akisaini kitabu cha wageni katika Usharika wa Mikanjuni Jimbo la Pwani.
Page 72 of 124


