Ikiwa leo tarehe 27/10/2024, katika  Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, ni Siku ya Kukumbuka Matengenezo ya Kanisa (Reformation) Askofu Dkt. Mbilu amesema kuwa Kanisa litaendelea kukemea mafundisho potofu yaliyotanda katika ulimwengu na kuendelea  kusimama katika msingi wa kuihubiri kweli ya Kristo.

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, amewasihi Wanawake kuchangamkia fursa mbalimbali zinazojitokeza katika jamii na Kanisa kwaajili ya kujikwamua kiuchumi ili kuondokana na umasikini pamoja na utegemezi.

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Dkt Msafiri Joseph Mbilu, amesema kuwa mwamko wa elimu katika Shule ya Sekondari Lwandai pamoja na Bangala Lutheran Junior Seminary ambazo zote zinamilikiwa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, umeongezeka zaidi ukilinganisha na hali ilivyokuwa hapo awali na kuwaomba wazazi na walezi kupeleka watoto wao katika Shule hiyo.

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, akiongoza Kikao cha Bodi ya Taasisi ya Elimu ya Kolowa Technical Training Institute (KOTETI),kilichofanyika Makao Makuu ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Lushoto Tanga tarehe 17/10/2024 ambacho kilijumuisha wadhamini wa mali za KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki.